Deutsche Welle: Serikali ya mpito ya Yemen imeufanyia marekebisho mswaada wa sheria ya kinga ya kutoshitakiwa kwa Rais Ali Abdullah Saleh na watu wake wa karibu.
Waziri Mkuu wa Misri Mostafa Madbouly amesema nchi hiyo itapokea awamu ya kwanza ya mkopo chini ya mkataba uliopanuliwa na Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF wiki ijayo.
Kiongozi wa kamati kuu ya mapinduzi ya Yemen Muhammad Ali Al-Houthi amesema kumekuwepo kwa mashambulizi aliyoyaita ya "kiholela" yaliofanywa na Marekani na Uingereza katika mji wa bandari wa Hodeidah nchini Yemen.
Vikosi vya Marekani vimesema vimeiharibu droni ya chini ya maji na karibu makombora 20 ya masafa marefu katika mfululizo wa mashambilizi dhidi ya waasi wa Houthi.