Deutsche Welle: Bingwa wa masumbwi ya uzito wa juu duniani Vitali Klitschko ameutetea ubingwa wake jana baada ya kumshinda Dereck Chisora wa Uingereza kwa pointi.
Katika michezo, nafasi ya kwanza inamaanisha ubingwa. Mbali na talanta unahitaji washauri na wakufunzi bora watakao kuongoza kufikia ubingwa. Hawa huchangia ushindi nyuma ya pazia na kumsaidia mchezaji kuvikabili vikwazo na ukiritimba unaojitokeza katika safari ya mashindano. #vijanamubashara
Mkenya Eliud Kipchoge anatarajia kuweka historia kwa kushinda medali yake ya tatu mfululizo ya Olimpiki ya mbio za marathon katika Michezo ya mwaka huu mjini Paris.
Bayern Munich wana nafasi ya kuyaweka hai matumaini yao ya kupata angalau taji moja msimu huu watakapotembelewa na Lazio hapo Jumanne katika mechi ya Ligi ya Vilabu Bingwa Ulaya, Champions League. Katika mechi ya raundi ya kwanza iliyochezwa huko Italia, Bayern walifungwa 1-0. Msikilize Bruce Amani akitoa tathmini yake kuhusiana na iwapo Bayern wataweza kukipindua kipigo hicho na wasonge mbele.