1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

14 wauawa na bomu Iraq

7 Januari 2008
https://p.dw.com/p/ClZ7

BAGHDAD:

Watu 14 wameuawa na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa katika milipuko miwili ya mabomu iliotokea mjini Baghdad jumatatu.

Miongoni mwa waliokufa ni kiongozi wa vijana wakujitolea kushika doria katika mtaa wa waarabu wa kisunni wa Adhamiya.Msemaji wa kundi la kidini linaloitwa Sunni Endowment,amesema kuwa mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijilipua karibu na lango kuu la jengo moja mahali hapo.Tena bomu lingine limelipuka karibu na hapo baada ya watu kukusanyika.